Botanix – Jarida kuhusu mimea

Toleo la Kiswahili

Mti wa mfune wa India Pongamia pinnata

foto

Pongamia pinnata

Mti wa mfune wa India Pongamia pinnata (majina mengine ya kienyeji: mti wa Honge, mtu wa Pongam, Panigrahi) una urefu wa takribani mita 15 –25, inapatikana kwenye familia ya Fabaceae. Ni mkubwa sehemu ya juu na maua madogo madogo mengi ya rangi nyeupe, waridi au urujuani. Asili yake ni India, lakini inaoteshwa kwa kiwango kikubwa Kusini – Mashariki mwa Asia.

Pongamia pinnata ni mti mgumu wa kitropika, una uwezo wa kujikinga na joto na mwanga wa jua. Una mfumo wa mzizi mkubwa na pia una uwezo wa kujikinga na ukame. Kwa kawaida, miti hii inakua vizuri kwenye udongo kichanga au udongo miamba, pamoja na mawe ya chokaa, lakini kwenye mashamba, inaweza kufanikiwa kukua karibu katika aina zote za udongo ikiwemo udongo wenye chumvi chumvi.

Mara chache inakua kwenye maeneo yenye ukame na mara chache inatumika kwa madhumuni ya kutunza mandhari kama kinga ya upepo au kwa ajili ya kivuli. Magamba yake yanatumika kutengenezea nyuzi au kamba, na utomvu umekuwa ukitumika huko zamani kutibu vidonda vilivyosababishwa na samaki wenye sumu.

Vinundu vya mizizi yake vinasaidia katika kuchochea naitrojeni, katika utaratibu wa kutegemeana ambapo naitrojeni yenye gesi (N2) kutoka kwenye hewa inabadilishwa na kuwa NH4+ (ambayo ni aina ya naitrojeni inayopatikana kwenye mmea). Hivyo, inaweza kutumika kurutubisha udongo wenye upungufu wa virutubishi. Ingawa mmea wote ni sumu, juisi na vile vile mafuta yanayotoka kwenye mmea huu ni antiseptiki. Mafuta yanayotokana na mbegu zake yanatumika kama mafuta ya taa, kutengenezea sabuni, kama mafuta ya kulainishia na pia kuzalishia dezeli.

««« Makala iliyopita: Shelisheli Artocarpus odoratissimus, Marang Makala inayofuata: Khasi Pine (Pinus kesiya) »»»

Jumamosi 8.8.2009 09:27 | chapa | Mimea ya kigeni

Kuhusu KPR

KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani Slovakia
KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani ni shirika la kimataifa la wakulima wa bustani. Soma zaidi...
Shirikisha uzoefu wako kuhusu ukuzaji mimea. Andika makala kuhusu ukulima wa bustani, mimea, upandaji wa mimea nk. na uichapishe kwenye toleo la lugha yako la jarida letu la Botanix! Wasiliana nasi kwa taarifa zaidi.